Add parallel Print Page Options

Kila wakati ninapowaombea ninyi nyote, daima ninawaombea kwa furaha. Ninamshukuru Mungu kwa namna mlivyonisaidia nilipokuwa ninawahubiri watu Habari Njema. Mlinisaidia tangu siku ya kwanza mlipoamini mpaka sasa. Nina uhakika kwamba Mungu, aliyeianzisha kazi njema ndani yenu, ataiendeleza mpaka itakapomalizika siku ile ambayo Kristo Yesu atakuja tena.

Read full chapter